Checklists

Kivunge cha Dharura & Orodha ya Mpangilio
Jinsi ya Kuhifadhi Maji ya Dharura – Lita
Lala chini, Jifunike na Ushikilie
Kadi ya Mawasiliano ya Eneo Mbali


Matukio ya dharura yanaweza kutokea wakati wowote. Katika eneo hili letu, matukio haya yanaweza kuwa dhoruba ya majira ya baridi, mafuriko ya maji, mitetemeko ya ardhi, mporomoko wa ardhi, sunami, moto, na uchafu hatari. Kujitayarisha wewe na familia yako kwa janga la aina yoyote ni muhimu kwa usalama wenu. Kuwa tayari kujitegemea kwa angalau siku tatu – zaidi ikiwa ni hali ya msiba mkubwa – kwani inaweza kuchukua siku kadhaa au wiki kadhaa kwa huduma muhimu kurejeshwa.

Kuna mambo maalum unayoweza kufanya ili kulinda wapendwa wako na mali yako wakati wa matukio ya dharura. Yanajumuisha:

Unda mpango – jua jinsi familia yako itawasiliana na mahali mtakutana ikiwa mtatenganishwa.

Unda kivunge cha dharura – jumuisha vitu muhimu, kama vile maji ya kunywa, vyakula vya kudumu, kivunge cha huduma ya kwanza, tochi, betri za ziada, redio inayotumia nishati ya kuzungusha mpini kwa mkono au betri, madawa ya maagizo ya daktari, nguo za joto na blanketi, na pesa taslimu. Usisahau vitu vya wanyama wako vipenzi pia!

Shughulika – juana na majirani wako na uwe tayari kusaidia wale huenda wakahitaji usaidizi, na ujifunze CPR/huduma ya kwanza.

Kuwa na taarifa – jisajili kwa arifa za eneo lako na za kanda, na usikilize idhaa za vyombo vya habari katika eneo lako.